top of page
Dr. Budodi

HAKUNA TIBA MBADALA INAYOTIBU PID

Tiba Mbadala ni mkusanyiko wa njia za matibabu ambazo ni tofauti na zile mbinu na dawa za kitaalamu kwa kuwa hizi huhusisha dawa au mbinu za asili za tiba kama vile matumizi ya dawa za mitishamba aina fulani ya vyakula na pia matumizi ya dawa fulani zilizotengenezwa moja kwa moja kutoka kwenye mimea au vyakula asilia. Tangu zamani mbinu na dawa hizi zimesaidia kutibu magonjwa mbali mbali na hata sasa zinaendelea kuokoa Afya na maisha ya watu.

dawa za BF suma

Aidha kukua kwa sayansi na Teknolojia kumeleta dawa na mifumo ya matibabu yenye ubora zaidi ya hizi. Matumizi ya dawa za hospitali ambazo hutolewa baada ya vipimo stahiki na kwa dozi stahiki kulingana na Umri, Uzito, Ukubwa wa tatizo na hali ya mgonjwa kiujumla. Tafiti mbali mbali zimefanyika katika nchi tofauti tofauti Duniani ikiwa ni pamoja na Tanzania na zikatambua na kufikia muafaka kuwa Dawa na Tiba za hospitali zinamatokeo mazuri zaidi na madhara kidogo sana ukilinganisha na Tiba m'badala. Hasa kwa upande wa magonjwa ya PID(maambukizi ya Bakteria kwenye Via vya uzazi vya mwanamke), Fangas wa sehemu za siri(VVC) na UTI (maambukizi ya bacteria kwenye njia ya mkojo.


Tafiti zinaonyesha matumizi ya tiba lishe zinazohusisha Asali,karafuu, mdalasini, Tangawizi, vitunguu swaumu, zabibu, Mchaichai, Chai, Rosmery na mkaratusi ambazo zinaweza changanywa na vilainishi pamoja na dawa kama Clotrimazole hazina ubora unaokaribia au kufikia Dawa za hospitali katika kutibu magonjwa haya. Matumizi ya tiba hizi hubadilisha dalili za ugonjwa tuu badala ya kutibu, kwa maana ya kwamba ikiwa mgonjwa wa P.I.D ambae alikua na dalili ya kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri pamoja na maumivu ya tumbo. Mgonjwa huyu akitumia tiba hizi atapata nafuu ya aidha kupunguza maumivu ya Tumbo au kuondoa harufu tuu lakini moja au mbili kati ya dalili hizi zitabaki na kuna uwezekano kuwa baada ya wiki 1 au 2 dalili zote zitarudia hali ya mwanzo.


karafuu, mdalasini


Maandalizi na utunzaji wa Dawa hizi ambazo hutumika kama Tiba mbadala hufanyika katika mazingira yasiyo na usimamizi na bila kufuata taratibu za kitaalamu za maandalizi. Hii huongeza uwezekano wa kupata dawa zisizo na viwango ambazo zinaweza leta madhara mengine ya kiAfya kwa watumiaji wamwisho. Kwa baadhi ya taasisi ambazo hufuata taratibu za kuandaa na kufungasha vizuri tiba hizi na hata kuthibitishwa na Shirika la chakula na Dawa - FDA, usambazaji wa dawa hufanyika na watu wasio na ujuzi wa kutosha hivo kupelekea makosa katika utunzaji na utoaji wa dozi sahihi kwa wagonjwa. Aidha watu hawa wasio na ujuzi wanaopewa nafasi ya kusambaza dawa hizi hawana uwezo wa kutosha kutambua magonjwa. Hii inapelekea makosa katika kutoa dawa sahihi kwa mgonjwa sahihi katika wakati sahihi swala ambalo linachangia kuongezeka kwa magonjwa ya figo na Ini.


Matumizi ya mtindi aidha kwa kupaka sehemu za siri au kunywa, pamoja na aina nyingine ya vichochezi kurudisha bakteria rafiki mwilini(probiotics) husaidia kupunguza dalili na kusaidia mwili kujikinga na  P.I.D(maambukizi ya Bakteria kwenye Via vya uzazi vya mwanamke), Fangas wa sehemu za siri(VVC) na UTI (maambukizi ya bacteria kwenye njia ya mkojo. Aidha probiotics hazitibu magonjwa haya zaidi ya kubadilisha dalili za ugonjwa husika swala ambalo linaweza leta changamoto katika kuutambua ugonjwa badae. Hivyo ni vema kutumia tiba stahiki za hospitali kutibu magonjwa haya.




MAAMBUKIZI YA BAKTERIA KWENYE KIZAZI KWA WANANAWAKE - PID


Utangulizi

PID ni maambukizi ya bakteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke kwa maana ya Mlango wa kizazi, Mji wa mimba, mirija ya uzazi pamoja na mayai. Bakteria wanaweza ingia kwa njia ya kushiriki tendo la ndoa, kuingiza vidole ama kitu chochote sehemu za siri ikiwa ni pamoja na Njia za uzazi wa mpango kama kitanzi kupitia uke wako. Si kila mwanamke mwenye PID huonyesha dalili kwani baadhi ya wanawake hujihisi wako sawa mpaka pale wanaposhindwa kubeba ujaa uzito au wanapokua na maumivu ya Tumbo chini ya kitovu kwa muda mrefu

maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na uchafu ukeni


Dalili za PID

  • Maumivu ya nyonga na Tumbo chini ya kitovu na

  • Kutokwa na uchafu mweupe, wa njano au wa kijani sehemu za siri wenye harufu kali (shombo ya samaki au yai bovu)

  • Maumivu wakati wa tendo

  • Maumivu wakati wa haja ndogo

  • Kubadilika kwa siku za hedhi na maumivu makali wakati wa hedhi

  • Homa na maumivu ya kichwa



Muda sahihi Kumuona Daktari

Unashauriwa kumuona daktari mapema baada ya kuona dalili zifuatazo

  • Harufu mbaya sehemu za siri inayoambatana na uchafu

  • Homa kali na kutapika

  • Maumivu makali ya tumbo chini ya kiovu


Unashauriwa kumuona Daktari hata ikiwa dalili za PID hazijawa kali kwakuwa kutokwa na harufu mbaya sehemu za siri, kubadilika kwa siku za hedhi au maumivu wakati wa tendo zinaweza kuwa dalili za magonjwa ya zinaa. Sitisha kushiriki tendo mpaka utakapo pata tiba sahihi ni vema kama wewe na mwenza wako mkatibiwa kwa pamoja



Vihatarishi vya kupata PID

  • Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

  • Kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi

  • Kushiriki tendo bila kutumia kondomu

  • Kupiga punyeto, hasa kwa kuingiza vitu ukeni huvuruga uwiano wa bacteria sehemu za siri

  • Historia ya kuwa na magonjwa ya zinaa



Madhara ya PID

Maambukizi haya husababisha vidonda, makovu na michubuko kwenye mfumo wa uzazi ambavyo vinaweza sababisha kutengenezwa kwa vifuko vya maji maji ambavyo hupelekea kutungwa kwa usaha kwenye mfumo wa uzazi na kuvuruga utendaji wa mifumo hiyo


  • Mimba kutunga nje ya kizazi; PID husababisha michubuko na pengine kutokea kwa vifuko vya usaha ndani ya mirija ya uzazi ambavyo vinaweza zuia yai kusafiri salaama mpaka kwenye mji wa mimba hivyo kusababisha mmba kutunga kwenye mirija ya uzazi. Ikigundulika mapema mrija husika hutakiwa kukata hali ambayo inaweza pelekea utasa na ikichelewa kutambulika inaweza sababisha kupasuka kwa mrija na mwanamke atapoteza damu nyingi kitu ambacho kinaweza sababisha kifo.


  • Utasa; Ikitokea umepata mimba ya nje ya kizazi zaidi ya mara moja utakatwa mirija yote na kuwa tasa. PID hushambulia via vya uzazi hivyo kuchelewa kupata tiba huongeza hatari ya utasa, wanawake waliougua PID zaidi ya mara moja wana hatari kubwa ya kuwa Tasa


  • Maumivu sugu ya Tumbo; Baada ya kushambulia via vya uzazi PID husababisha makovu na michubuko hali ambayo inaweza pelekea maumivu ya tumbo yasiyoisha kwa miezi mpaka miaka


  • Kuziba kwa mirija ya uzazi na kutunga usaha; Baada ya kushambuliwa mirija ya uzazi inaweza kutunga maji maji au usaha ambao unasababisha mirija kuziba. Maranyingi usaha hushambulia mirija lakini pia unaweza athiri mji wa mimba na mayai



Jinsi ya Kujikinga na PID

  • Shiriki ngono salaama kwa kutumia kondomu

  • Epuka punyeto

  • Epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na epuka kuwa na mpenzi mwenye mahusiano mengi

  • Epuka matumizi ya njia za uzazi wa mpango za Hormone







54 views1 comment

1 Comment


Tanzanite boy
Tanzanite boy
6 days ago

Asaante sana Daktari, Sikuwahi jua mambo yako hivi

Like
bottom of page